VYOMBO
( ASASI ) MBALI MBALI VYA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI NCHINI
Baada ya uhuru, serikali imechukua hatua
mbali mbali ili kukuza na kueneza Kiswahili . hatua moja wapo ni ile ya kuunda
asasi za ukuzaji Kiswahili. Asasi hizo
ni:
1.
UKUTA
Hiki ni chama cha Usanifu wa Kiswahili na
Mashairi . chama hiki kilianzishwa mwaka 1965 na mshairi Mathias Mnyapala kwa
lengo la kukuza ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.
Ukuta ilikuwa na malengo yafuatayo:
a). Kukuza lugha ya Kiswahili na ushairi
kwa ujumla kwa njia ya kujishughulisha na kazi tafauti zinazohusiana na
maendeleo ya Kiswahili na ushairi kama vile uhariri wa miswada ya Kiswahili,
utunzi wa mashairi na uandishi wa vitabu na kutafsiri maandishi mbali mbali
katika Kiswahili.
b).
Kukuza utunzi wa ngonjera na kuhamasisha utunzi wa vitabu katika misingi
yenye kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
Mafanikio ya
UKUTA.
c).
Imeweza kuundaa na kuendesha semina na makongamano ya Kiswahili na
kutunga kazi za fasihi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
d).
UKUTA imeweza kuandika vitabu mbali mbali vya ushairi hususan vya ushairi,
kama vile Ngonjera za ukuta ( cha kwanza
na cha pili - 1968 ), Mashairi ya Azimio la Arusha – 1974 na Mashairi ya miaka
kumi ya Azimio la Arusha – 1977.
e).
Imeweza kutafsiri kwa Kiswahili maandishi mbali mbali . mfano , iliwza
kutafisiri majina ya baadhi ya mitaa ya jiji la Dar – es – Salaam kama vile
mtaa wa uhuru badala Independence Avenue na mtaa wa Sokoine badala ya Sokoine
Drive.
2.
TUKI ( Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili ).
Taasisi hii kihistoria ilianzishwa mwaka
1930 ikiwa kamati ya lugha ya lugha ya Afrika Mashariki na uatwala wa
Waingereza , na mnamo mwaka mwaka 1964, ilipandishwa hadhi na kuhamishiwa
katika chuo kikuu cha Dar –es – Salaam baada ya kuimarishwa kwa sheria ya Bunge
ya mwaka 1964. Na mwaka 1970 kilipoanzishwa chuo kikuu cha Dar –es Salaam
taasisi ilikuwa moja wapo wa asasi za utafiti wa chuo, ambapo mpaka leo asasi
hii imekuwa ikifanya kazi chini ya Chuo Kikuu,
Mnamo mwaka 2009, taasisi hii ilibadili
jina baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili ya chuo na kujulikana kwa jina la
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. ( TATAKI ).
Malengo ya TUKI ( TATAKI ).
i). Kuichunguza na kuiendeleza
lugha ya Kiswahili katika fani zake zote ikizingatia mipango ya muda mrefu
katika Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Afrika na mashariki na Katika chuo kikuu
cha Dar es Salaam.
3.BAKITA
( Baraza la Kiswahili Tanzania).
Baraza hili liliundwa mwaka 1967 kaw
sheria ya Bunge Na. 27. Ya mwaka huo.
Malengo
makuu ya uundwaji wa baraza hili ni kutaka kuwepo kwa chombo nchini cha
kusimamia shughuli za ukuzaji Kiswahili.
KAZI
ZA BAKITA.
i). Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha,
kuandika vitabu vya Kiswahili na taaluma zake hususan fasihi na sarufi.
ii).
Kutoa huduma za ukalimani kwa serikali na mashirika
iii). Kuratibu kazi za ukuzaji Kiswahili
nchini na zile zinazofanyika nchi za nje.
iv). Kuchapisha majarida ya Kiswahili
yatakayoongoza matumizi sahihi ya maneno na maendeleo yake.
v). Kuchunguza usahihi wa lugha ya
Kiswahili inayotumika katika uandishi wa vitabu mbali mbali vinavyokusudiwa
kutumika kufundishia shuleni na vyuoni kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu.
vi). Hujishughulisha na uthibitishaji wa
tafsiri sanifuza isitilahi na kusimamia utafiti wa lugha ya Kiswahili.
vii). Kutoa ushauri kwa waandishi na
wachapishaji kuhusu utumiaji wa Kiswahili fasaha na kuratibu maendeleo ya
Kiswahili nchini.
Katika utekelezaji wa shughuli zake,
baraza hilo limeanzisha idara tano za taaluma. Nazo ni:
§ Idara ya Uhariri na Uchapishaji.
Idara hii hujishughulisha na masuala mbali mbali ya uchapaji wa taarifa za
BAKITA na majarida mengine.
§ Idara
ya Lugha na Fasihi.
Idara hii husimamia matumizi sahihi ya
Kiswahili sanifu katika vyombo vya habari
na matumizi rasmi na kutoa ithibati ya vitabu vya Kiswahili
vinavyokusudiwa kutumika katika elimu.
§ Idara ya Tafsiri na Ukalimani.
Idara hii hujishughulisha na kutoa
huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha ya Kiswahili kwa
mashirika,idara,wizara,balozi na watu binafsi.
§ Idara ya Istilahi na kamusi.
Hii inafanya kazi
ya kufanya tafiti za isitilahi, kuandaa orodha ya isitilahi na kuandaa kamusi
kwa matumizi ya asasi, shule na watu wa aina mbali mbali.
§ Idara
ya Uhusiano
Idara hii inafanya kazi ya kutangaza
kazi za shughuli za baraza kwa kutumia radio,magazete na majarida na kusimamia
vipindi vya Kiswahili katika radio na televisheni, pamoja kuimarisha uhusiano
baina ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili kwa kuandaa warsha na semina.
MAFANIKIO
YA BAKITA
. Bakita imeandaa isitalahi za taaluma mbali
mbali kama vile za Fizkia, Kemia, Uchumi, Ufundi, Bunge , maktaba n.k
. Bakita inatoa majarida mbali mbali yanayohusu
lugha ya Kiswahili kama vile lugha yetu tusome tuijue, jifunze Kiswahili
uwafunze wengine , lugha ya kiswahili – fasihi na sarufi yaken.k
. Bakita huendesha vipindi mbali mbali vya
Kiswahili katika radio Tanzania dar es sallam
kama vile lugha yetu, ulimwengu wa Kiswahili, Kiswahili lugha ya taifa
n. k
MATATIZO
YA BAKITA.
a. Uhaba
wa fedha wa kuendeshea shughuli za bakita, kama vile warsha ,semina,makongamano
uchapishaji wa majirida.
b. Uhaba
wataalamu
4).
TAASISI YA KISWHILI NA LUGHA ZA KIGENI. ( TAKILUKI ).
Taasisi hii iliundwa mwaka 1979 ikiwa chini
ya Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali
Zanzibar.
Lengo kubwa ya kuanzishwa taasisi hii ni
:Kusimamia na kuendeaha shughuli za ukuzaji wa kiswahli na lugha za kigeni
kisiwani humo.
KAZI
ZA TAKILUKI:
a. Kutoa
mafunzo na elimu ya Kiswahili kwa kiwango cha juu kwa watumishi wa serikali na
viongozi wa chama ua vyama ili kukuza ujuzi wa Kiswahili na kuzumgumza Kiswahili fasaha
b. Kufanya
utafiti wa Kiswahili , kuandika vitabu vya taaluma mbali mbali za Kiswahili na
kutafsiri katika kisahili maandishi mbali mbali yaliyo katika lugha za kigeni.
c.
Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha ,
kuchapisha vitabu vya Kiswahili na
kuwapa waandishi chipukizi miongozo ya uandishi sahihi wa vitabu.
d. Kuratibu
na kusimamia maendeleo ya Kiswahili visiwani Zanzibar pamoja na kuendesha
mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni
e. Kuandaa
isitalahi za taaluma mbali mbali pamoja na kutoa huduma za tafsiri na ukalimani
kwamashirika ,idara wizara kampuni,na watu binafsi , pia hufundisha lugha za
kigeni kama vele GR, PR FR ARB CHINA na kuandika vitabu vya Kiswahili.
f.
Hujishughulisha na ufuatiliaji pamoja
na usimamizi wa matumizi sahihi ya Kiswahili katika vyombo vya habari katika
shughuli mbali mbali za serkali na za kawaida.
g.
Kufanya utafiti wa lahaja na fasihi
simulizi ya Kiswahili.
MAFANIKIO YA TAKILUKI.
Takiluki imepata mafanikio kadhaa yakiwemo haya yafutayo:
1.
Kuchapisha vitabu mbali mbali vya Kiswahili
kama vile malenga wapya, na tungo zakale.
2.
Kuandaa na kuendesha semina na
makongamano mbali mbali ya Kiswahili.
3.
Kuhimiza ufundishaji wa Kiswahili
visiwani Zanzibar.kushirikiana na vyombo mbali mbali vyaukuzaji lugha ya
Kiswahili katika kutekeleza mipango mbali mbali ya ukuzaji Kiswahili.
BAKIZA.
( BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR ).
Ni chombo chengine ambacho kimesidia
kukuza na kustawisha kugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar. Baraza hili
lilianzishwa mwaka 1983.
KAZI
ZA BAKIZA.
·
Kuratibu na kusimamia maendeleo ya
Kiswahili visiwani Zanzibar.
·
Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha
na kufanya utafiti wa Kiswahili kwa kushirikiana na vyombo vingine.
·
Kuendesha semina za Kiswahili na
kuwafundisha waandishi misingi ya uandishi.
·
Huratibu maendeleo ya Kiswahili na
kutoa ushauri kwa serikali kuhusu namna ya kufanikisha ukuzaji wa Kiswahili
ndani nan je ya Zanzibar.
CHAMA
CHA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Chama hiki kilianzishwa mwaka 1970
kwa juhudi za mwanzo za wanafunzi walioingia chuo kikuu kusoma Kiswahili katika
ngazi ya shahada ya kwanza.
Chombo hiki kilikuwa na madhumuni
yafuatayo:
·
Kuwapa wanachama nafasi ya kuvumbua na
kukuza vipawa vyao katika isimu na fasihi ya Kiswahili.
·
Kuamsha ari ya kimapinduzi katika
kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa njia ya uchunguzi namaandishi.
MAFANIKIO
YA CHAMA HIKI.
a. Kutoa
jarida ya kioo cha lugha.
b. Kutoa
nafasi kwa walimu na wanafunzi kujadili na kuhakiki fani mbali mbali za isimu
na fasihi.
c.
Kuongoza makongamano ambayo mijadala
yake huhaririwa na kutolewa katika kijarida kiitwacho ZINDUKO.
TAASISI
YA ELIMU.
Taassisi hii ilianzishwa mwaka 1966 na ilikuwa na kazi zifuatazo:
a. Kutayarisha
mihutasari ya masomo ya shule za msingi na sekondari pamoja vyuo vya elimu.
b. Kutayarisha
na kuongoza semina mbali mbali kwa
walimu ili waweze kufundisha vyema lugha ya Kiswahili.
c.
Kutoa muongozo mpya kuhusu utahini wa
somo la Kiswahili katika kidato cha tatu na nne wakishirikiana na baraza la
mitihani la taifa.
MAFANIKIO
YA TAASISI HII.
·
Kuandaa mihutasari ya masomo mbali
mbali hapa nchini.
·
Kuandaa vitabu vya kufundishi Kiswahili
sekondari kama vile Kiswahili kidato cha 1 – 4 (1996).
TAASISI
YA ELIMU YA WATU WAZIMA.
Taasisi hii ilianzishwa mwaka 1963. Kama
chombo cha kuwasaidia wazelendo katika
stadi za kusoma na kuandika ambao hawakupata fursa ya kupata elimu katika ngazi
ya msingi na sekondari.
Baadhi ya mafanikio ya elimu ya watu wazima
ni:
·
Kufanikiwa kutoa elimu ya watu wazima
katika stadi za kusoma na kuandika wakati wa jioni kwa lengo la kufuta ujinga .
·
Kutoa masomo kwa njia ya posta kwa
kidato cha kwanza hadi cha sita katika somo la Kiswahili.
·
Kuanzisha maktaba makao makuu ambayo
huwasidia wanafunzi kupata vitabu na majarida mbali mbali ya Kiswahili.
·
Kunzisha idara ya mafunzo ya elimu ya
watu wazima ambapo wanafunzi kutoka ndani na n je ya nchi husomea diploma ya
elimu ya watu wazima.
IDARA
YA KISWAHILI – CHUO KIKUU DAR ES SALAAM
Idara hii ilianzishwa mwaka 1970 baada ya
kuanzishwa chuo kikuu.
Kazi kubwa ya idara hii ilikuwa ni:
·
Kutayarisha walimu na wataalamu wenye
shahada katika somo la Kiswahili ili waweze kufundisha mashuleni na vyuoni.
Mafanikio makubwa ya idara hii ni kuweza
kutoa walimu wengi wenye shahada ya
Kiswahili wanaofundisha mashuleni mashuleni na vyuoni,
Pia imeweza walimu wenye shahada ya pili , tatu na hata uprofesa wa lugha ya kiswahili.
CHAMA
CHA KISWAHILI CHA AFRIKA.
Chama hiki kiliundwa katika semina ya
kimataifa kuhusu usanifishaji wa isitilahi za Kiswahili iliyofanyika chuo kikuu
dar es salaam mwaka 1978. Ikiwa na wajumbe tafauti waliotoka nchi za Kenya,
Tanzania, msumbuji, na Zambia ikiwa na madhumuni yafuatayo:
·
Kukuza kueneza Kiswahili kote afrika.
·
Kuleta umoja katika mataifa ya kiafrika
kwa kutumia lugha ya asili.
Pia
semina nyengine iliandaliwa tena mwaka 1983 na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka
Kenya, Rwanda, Comoro, Uganda, DRC, Zanzibar na kutoka radio mbali mbali kama vile India,
BBC, RTD, Radio Rwanda n.k na waliazimia mambo yafuatayo:
·
Kuandaa mikutano ,semina na warsha zitakazotumika kuchambua isitilahi za
Kiswahili badala ya kawaachia Tanzania peke yake.
·
Kusambaza isitilahi za Kiswahili
zitumike na watu wa kawaida na hasa wale wanaojishughuisha na ukuzaji Kiswahili
ndani na nje ya mipaka yake.
·
Kupendekeza mpango wa usanifishaji wa
isitilahi uwe wa kiwango cha kimataifa.
·
Kuanzisha jarida makhsusi ambalo
litajidili masuala ya usanifishaji ili kuimarisha taasisi mbali mbali zinazo jishughulisha
na Kiswahili kama vile unesco.
MATATIZO
YA CHAKA.
·
Kuachiwa Tanzania peke yake katika usanifishaji
wa isitilahi.
·
Kutafsiriwa kwa maneno ya kigeni bila
ya utafiti mkubwa ambayo hupelekea kutokuwa na mvuto kwa wasomaji wa kawaida.
·
Kutokuwa na msukumo wa viongozi wa nchi
wanachama kwani viongozi wengine walipiga vita shughuli hii badala ya kutoa
ushauri na kuhimiza.
UWAVITA.
( Umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania ).
Umoja huu ulianzishwa mwaka 1974 na ulikuwa
na madhumuni yafuatayo:
·
Kuwahimiza watu kuandika vitabu mbali
mbali vya Kiswahili.
·
Kuwasidia waandishi chipukizi ikiwa ni
pamoja kuwafahamisha uandishi wa masuala mali mbali ya fasihi.kujishughulisha
na kukikuza na kukitangaza Kiswahili katika vyombo vya habari kama vile radio
na magazeti.
·
Kutetea maslahi ya waandishi wa
kitanzania ili kuwaunganisha pamoja.
·
Kubuni na kuendesha miradi ya
uandisshi, uchapaji na uchapishaji.
·
Kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa
kusoma, uandishi wa vitabu na Sanaa zinazoambatana nazo kwa njia ya radio na
magazeti.
TATHMINI
YA MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU.
Lugha ya Kiswahili baada ya uhuru
imepata mafanikio kadhaa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:
a. Uendelezwaji
wa Kiswahili.
Kiswahili kimeweza kuendelezwa kwa njia
mbali mbali kama vile kufundisha kama somo moja wapo katika ngazi zote za elimu
nchini, kufanyiwa utafiti, kusanifiwa na kutumika kama lugha kuu ya
mawasiliano.
b. Kuongezeka
kasi ya ueneaji wa lugha ya Kiswahili.
Kiswahii kimeweza kuenea hadi nje ya
Tanzania katika mataifa mbali mbali na hata kufikia moja wapo lugha ya
kimataifa na pia kuongezeka msamiati.
c.
Kuongezeka kwa uundwaji wa vyombo vya
ukuzaji Kiswahili.
Kuendelea kujitokeza vyombo mbali mbali vya
ukuzaji wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania
ni mafanikio makubwa kwa upande wa lugha ya Kiswahili kwa sababu vyombo
hivyo vimewea kuikuza lugha ya Kiswahili kwa njia mbali mbali.
d. Kutumika
Kiswahili katika vyombo vya habari vya nje.
Kuendelea kutumika lugha ya Kiswahili katika vyombo mbali mbali vya
habari vya nje kama viel BBC. Deutchwelle,radio japani, sauti ya amerika na
nyinginezo kumeifanya lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha mashuhuri
duniani
CHANGAMOTO
ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI.
Pamoja na mafanikio hayo ,zimekuwapo
changamoto kadhaa zinazoathiri maendeleo ya Kiswahili. Baadhi ya changamoto
hizo ni:
·
Upotoshwaji wa lugha ya Kiswahili.
Upotwashwaji wa Kiswahili hutokea kwa namna kadhaa mfano ni wa
uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno
yasio yanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za
kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.
·
Athari za lugha za kigeni.
Tatizo la
kutokithamini Kiswahili miongoni mwa wanajamii ni changamoto ya kuathiriwa na
kasumba za ukoloni ambapo wanajamii huthamini Zaidi lugha za kigeni hususan
kingereza.
·
Kutokuwepo uwiano wa kimatumizi.
Hii ni
changamoto nyengine ambapo Kiswahili hakina uwiano wa kimatumizi katika nchi
nzima, tofauti hizi zipo kutokana na jamii moja na nyingine kuathiriwa na lugha
mama.
·
Utafauti wa sera .malengo na mipango ya
vyombo vya ukuzaji Kiswahili.
Juhudi za ukuzaji Kiswahili zinaonekana
hazina mashiko kutokana na kuwepo idadi kubwa ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili
ambayo havina mshikamano wa pamoja kwani kila chombo kina malengo,sera, na
mipango ya yake ya uendeshaji wa Kiswahili.
·
Uhaba wa wataalamu.
Uhaba wa wataalamu katika vyombo vya ukuzaji
wa Kiswahili husababisha vyombo kutofanya
na kutekeleza malengo kwa ufanisi.
·
Kutokwepo mpango wa kukitumia Kiswahili
kama lugha ya kufundishia.
Ni tatizo jengine linalokwanishwa maendeleo
ya Kiswahili kwa kutotekelezwa kwa mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya
kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini, na hivyo kutoa mwanya hasa kwa
lugha za kigeni kama vile kingereza kustawi zaidi na hivyo kuathiri nafasi ya
Kiswahili katika jamii.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments: